#Football #Sports

SOFAPAKA YAKABILIWA NA HATARI YA KUSHUKA

Aliyekuwa kocha wa Harambee Stars, Twahir Muhiddin, amesema Sofapaka FC inahitaji “muujiza” ili kuepuka kushuka daraja katika Ligi Kuu ya FKF.

Muhiddin ameeleza kuwa vita vya kushuka daraja bado viko wazi huku timu kadhaa zikiwa hatarini msimu ukikaribia tamati.

Sofapaka iko mkiani mwa jedwali ikiwa na alama 15, alama 10 nyuma ya Kariobangi Sharks, ikiwa zimesalia mechi tisa pekee, hali inayowapa kibarua kigumu kujiokoa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *