ULINZI STARS WAPIGA HATUA DHIDI YA KUSHUKA DARAJA
Ulinzi Stars wamejiweka katika nafasi nzuri ya kupambana na kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nairobi United katika mechi ya Ligi Kuu ya msimu wa 2025/2026.
Ingawa ushindi huo umepunguza presha ya haraka, timu hiyo bado iko kwenye vita vikali vya kusalia ligini, huku timu tatu za mwisho zikikumbwa na hatari ya kushuka daraja moja kwa moja bila nafasi ya mchujo.
Mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Police Sacco pia ilishuhudia mwanzo mpya kwa klabu hiyo, huku kocha wa muda James Mulinge Ndeto akiongoza kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka kwa Stephen Ocholla.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































