UJIO WA AUMA WATARAJIWA KUIMARISHA LIONESSES
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya raga Kenya Lionesses Simon Odongo, ameonyesha Imani ya kuimarika kwa kikosi chake kutokana na kurejea kwa Judith Auma, timu hiyo inapojiandaa kwa mkondo wa pili HSBC SVNS Div 2 jijini Montevideo, Uruguay wikendi hii.
Half-back huyo wa Impala RFC anarejea kutoka mkekani kutokana na jeraha la muundi wa mguu, ambalo lilimweka nje ya kipute cha Safari Sevens, Africa Cup Series, na mkondo wa kwanza wa HSBC Series jijini Nairobi, ambako Lionesses walimaliza katika nafasi ya 5.
Odongo anaamini kwamba ubunifu wa mchezaji huyo utakuwa muhimu katika kuimarisha mashambulizi ya kikosi hicho.
Lionesses watafungua mkondo wa pili dhidi ya Uchina Jumamosi, kabla ya kuvaana na Argentina na Uhispania siku hiyo.
Jumapili watacheza na Afrika Kusini na Brazil kukamilisha mkondo w Montevideo, kabla ya kuelekea Sao Paulo, Brazil wiki ijayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































