#Football #Sports

KATIBU MKUU WA CAF AJIUZULU

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Afrika, Veron Mosengo-Omba, amejiuzulu katika kipindi chenye misukosuko kwa mchezo huo barani.

Katika taarifa yake, Mosengo-Omba ametangaza kustaafu, huku uamuzi huo ukijiri wakati shirikisho hilo linakosolewa vikali kufuatia maamuzi tata, yakiwemo kuinyang’anya Senegal ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 na kuahirishwa kwa mashindano ya wanawake katika dakika za mwisho.

Amesema anaondoka akiwa na dhamiri safi baada ya kushughulikia tuhuma zilizomkabili, akiongeza kuwa anaamini ameimarisha taasisi hiyo licha ya changamoto na mizozo iliyoshuhudiwa katika kipindi chake cha uongozi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *