KWS YAKANA KUHUSIKA NA KUTOWEKA KWA MVUVI
Shirika la kutoa hifadhi kwa wanyamapori nchini, KWS, limeendelea kujitenga na madai ya kuhusika katika kutoweka kwa mvuvi Brian Odhiambo katika mbuga ya Lake Nakuru mwanzoni mwa mwaka jana.
Akiwa mbele ya kamati ya seneti kuhusu usalama, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Erastus Kanga, ameiambia kamati hiyo kwamba Odhiambo, anayedaiwa kukamatwa na maafisa wa KWS, hayuko kwenye rekodi za shirika hilo.
Walalamishi sasa wanataka uvuvi kwenye mbuga hiyo kuhalalishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































