MAHAKAMA YA JUU YATETEA UHALALI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA
Mahakama Kuu imeidhinisha uhalali wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF) huku ikibaini kuwa utekelezaji wake kitaifa haukuzingatia viwango vya kikatiba kutokana na mapungufu ya kiutaratibu na kiutendaji.
Katika uamuzi wake, Jaji Bahati Mwamuye amesema kuwa ingawa mfumo wa kisheria unaouongoza mfuko huo ni thabiti, namna ulivyotekelezwa ilikiuka haki muhimu za kikatiba ikiwemo haki ya utu na huduma ya afya.
Kesi hiyo iliwasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah aliyepinga uhalali wa mfuko huo pamoja na mchakato wa utekelezaji wake, huku mahakama ikithibitisha kuwa vifungu vinavyoanzisha mifuko ya huduma ya afya ya msingi, bima ya afya ya jamii na huduma za dharura pamoja na magonjwa sugu ni halali kikatiba.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































