OYUU APUUZA AZMA YA SOSSION KNUT
Katibu Mkuu wa KNUT Collins Oyuu amepuuzilia mbali azma ya mtangulizi wake Wilson Sossion ya kugombea katika uchaguzi ujao wa kitaifa wa chama hicho.
Oyuu amesema kuwa Sossion kwa sasa si mwanachama wa chama hicho, hivyo hana sifa za kushiriki katika uchaguzi wa ndani wa KNUT.
Kauli hiyo inaibuka huku kukiwa na mjadala kuhusu uongozi wa chama hicho, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa kufuata katiba na kanuni za chama katika uchaguzi wake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































