#Local News

MAIGIZO YA POLISI NJE YA AFISI YA SAKAJA

Maswali yameibuka kuhusu ni kwanini maafisa wa polisi wakaamua kumsaka gavana wa Nairobi Johnson Sakaja afisini kwake jana usiku baada ya saa za kazi, licha ya kamati ya seneti kuhusu uhasibu kutaka gavana huyo awasilishwe mbele yake jana saa nne asubuhi.

Katika kinachoonekana kama maigizo, makumi ya polisi wakiongozwa na msemaji wa polisi Muchiri Nyaga na kamanda wa polisi eneo la Nairobi Issa Mohamud, walikita kambi nje ya afisi ya gavana huyo jana usiku wakilenga kumkamata, muda mrefu baada ya kamati hiyo kumwagiza Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja afike mbele yake.

Haya yanajiri baada ya Sakaja kufeli kufika mbele ya kamati hiyo kujibu maswali kuhusu uhasibu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *