#Football #Sports

AROKO ALENGA KUOKOA KARIOBANGI SHARKS

Mshambuliaji chipukizi wa Kariobangi Sharks, Humphrey Aroko, amesema lengo lake kuu ni kusaidia timu hiyo kuepuka kushuka daraja katika Ligi Kuu ya Kenya.

Aroko alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari baada ya kuonyesha kiwango bora na kufikisha mabao 12 hadi sasa msimu huu. Hata hivyo, amesema mafanikio hayo binafsi si muhimu sana kulinganisha na malengo ya timu.

Aidha Ameeleza matumaini kuwa tuzo hiyo itampa motisha ya kuendelea kung’ara, hasa katika mechi ijayo dhidi ya AFC Leopards Jumapili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *