AJALI YA TRENI UFARANSA – MTU MMOJA AFARIKI
Dereva wa treni ya abiria ya mwendo wa kasi amefariki baada ya treni hiyo kugongana na lori lililokuwa limebeba vifaa vya kijeshi katika kivuko cha reli nchini Ufaransa.
Watu kadhaa wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea kati ya miji ya Béthune na Lens katika eneo la Pas-de-Calais kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa, watu wawili walipata majeraha mabaya huku wengine kumi na mmoja wakijeruhiwa kwa kiwango kidogo, huku Rais wa eneo hilo Xavier Bertrand akithibitisha kifo hicho na kueleza ajali hiyo kuwa ni janga kubwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































