NAIROBI KUPATA SURA MPYA
Jiji la Nairobi limeratibiwa kupata mwonekano mpya kufuatia kutia saini kwa makubaliano ya kuanzisha kwa ukumbi wa kisasa wa michezo na burudani katika eneo la reli katikati mwa jiji, ambao umeratibiwa kukamilika ndani ya miezi 12 ijayo.
Mradi huo utakaogharimu mabilioni ya pesa unalenga kuipa kaunti ya Nairobi sura mpya na kuiwezesha kushindana na miji mingingine.
Hafla ya kutiwa saini imeongozwa na rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































