WAKAZI WALIA KUHUSU AJALI MATISI – TRANS NZOIA
Wakazi wa eneo la Matisi katika Kaunti ya Trans Nzoia wamelalamikia ongezeko la ajali katika barabara kuu inayoelekea mpaka wa Suam nchini Uganda.
Wamesema kuwa katika kipindi cha chini ya miezi sita, zaidi ya watu kumi na sita wamepoteza maisha baada ya kugongwa na magari yanayokwenda kwa mwendo wa kasi, hali inayozua hofu miongoni mwa wakazi.
Wakazi hao sasa wanaiomba serikali kuchukua hatua za haraka, zikiwemo kudhibiti mwendo wa magari na kuimarisha usalama wa watumiaji wa barabara hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































