VIRGIL VAN DIJK AOMBA RADHI MASHABIKI WA LIVERPOOL
Virgil Van Dijk amewaomba radhi mashabiki wa Liverpool baada ya kukiri kuwa timu yake ilikata tamaa katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City.
Timu ya Arne Slot ilipoteza 4-0 katika Uwanja wa Etihad Jumamosi, jambo lililomfanya Van Dijk kuchukizwa na kiwango cha nusu ya pili.
Liverpool walikuwa nyuma 2-0 nusu ya kwanza baada ya mabao ya Erling Haaland, na kukubali bao mara moja baada ya kuanza kwa nusu ya pili wakati Antoine Semenyo alifunga na Haaland kukamilisha hat-trick yake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































