MELI YA KENYA MV SEA MFALME YAZUILIWA TANZANIA
Mamlaka ya usafiri wa baharini nchini (KMA) imethibitisha kuwa meli yenye bendera ya Kenya Imezuiliwa nchini Tanzania.
Katika taarifa yake, KMA imesema kuwa meli hiyo kwa jin MV Sea Mfalme imezuiliwa nchini Tanzania na kuwa inafanya mashauriano na idara za serikali katika mataifa yote mawili ili hatua mwafaka ziweze kuchukuliwa.
Mamlaka hiyo imewahahikishia washikadau katika sekta ya baharini kuwa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitatolewa na kuwa tayari hali hiyo inashughulikiwa ndani ya sheria za kiserikali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































