POLISI WASHUTUMIWA KWA MAUAJI EMBU
Gavana wa Embu Cecil Mbarire, ameshinikiza uchunguzi huru katika tukio ambapo maafisa wa polisi wanaripotiwa kuwaua watu 3 kwa kuwafyatulia risasi na kuwajeruhi wengine kadhaa wakati wa maandamano katika eneo la Ishiara, Mbeere North.
Wakazi wamesema polisi walitumia nguvu kupita kiasi kudhibiti maandamano hayo ya hapo jana yaliyolenga kushinikiza utendakazi bora katika hospitali ya Ishiara Level 4.
Kupitia taarifa, amesema serikali yake imeanzisha mchakato wa kuangazia masuala yaliyoibuliwa kuhusu hospitali hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































