#Local News

KIKOSI MAALUM KUWADHIBITI WAHUNI, MURKOMEN

Serikali imelazimika kutumia kikosi maalum cha polisi kukabili makundi ya wahuni ambayo yamechipuka katika maeneo mbali mbali ya nchi na kutatiza mikutano ya kisiasa hasa ya viongozi wa upinzani.

Akizungumza katika kaunti za Trans Nzoia na Nandi, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, amesema amemwagiza Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja kutuma kikosi hicho, akiwalaumu wanasiasa kutokana na kuchipuka kwa makundi hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *