OGAMBA: SERIKALI IMETATUA DENI LA WACHAPISHAJI VITABU
Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba amesema serikali imetatua mzozo wa deni la wachapishaji vitabu, hatua inayofungua upya mchakato wa uchapishaji na usambazaji wa vitabu shuleni.
Ogamba amesema Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni tano nukta sita, fedha zitakazowezesha kuendelezwa kwa shughuli za uchapishaji zilizokwama kwa muda.
Waziri huyo ameongeza kuwa Wizara ya Elimu inatarajiwa kutuma barua kwa wachapishaji ili waanze mara moja uchapishaji na usambazaji wa vitabu katika shule mbalimbali nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































