FAITH KIPYEGON KUANZA MSIMU SHANGHAI
Mwanariadha mashuhuri wa Kenya Faith Kipyegon anatarajiwa kuanza msimu wake wa 2026 kwa kushiriki mbio za mita 5,000 katika ufunguzi wa mashindano ya Diamond League utakaofanyika mjini Shanghai/Keqiao tarehe 16 Mei.
Bingwa huyo mara tano wa Diamond League anarudi China kwa mwaka wa pili mfululizo, ambapo ataongoza mbio hizo za mita 5,000 katika mashindano hayo ya ufunguzi.
Tangu mwaka 2023, Kipyegon ameweka rekodi tano mpya za dunia katika mbio tofauti kwenye miji mbalimbali ya Diamond League, akithibitisha ubora wake katika riadha.
Hata hivyo, mbio za mita 5,000 katika tukio la Keqiao zitakuwa za ziada, hivyo hatapata alama za kuwania msimamo wa Diamond League.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































