#Local News

RUTO: UDA-ODM BADO PAMOJA

Rais William Ruto amekariri kuwa vyama vya UDA na ODM vitaendelea kushirikiana kupitia mpango wa serikali jumuishi yaani Broad-based ili kufanikisha mageuzi nchini.

Kulingana na Ruto, ni kupitia ushirikiano huo ndipo wananchi katika maeneo mbali mbali watafikiwa na maendeleo, akiwaonya viongozi wa upinzani dhidi ya kauli zao anazosema zitalitumbukiza taifa katika machafuko.

Amehimiza ukomavu wa siasa nchini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *