PETROLI, DISELI YAVUKA SH.200 KWA LITA
Wakenya sasa watalazimika kuingia mfukoni zaidi kugharamia mahitaji ya kila siku kama vile chakula na usafiri, baada ya serikali kupandisha bei ya petroli kwa shilingi 28.69 kwa lita na diseli kwa shilingi 40.30, bei hiyo ikitekelezwa kwa kipindi cha tarehe 15 Aprili na tarehe 14 mwezi ujao.
Kulingana na taarifa ya mamlaka ya kudhibiti kawi na bidhaa za petroli, EPRA, lita moja ya peroli itauzwa kwa shilingi 206.87, diseli kwa shilingi 206.84 huku lita moja ya mafuta taa ikisalia shilingi 152.78 jijini Nairobi.
EPRA imesema mabadiliko hayo ya bei yamechangiwa na kupanda kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la kimataifa sawa na ukosefu wa udhabiti katika ubadilishanaji wa sarafu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































