CHAMA CHA WAMILIKI WA MATATU KIMETHIBITISHA MPANGO WA KUONGEZA NAULI
Rais wa Chama cha Wamiliki wa Matatu Albert Karakacha ametangaza kuwa bei za nauli za magari ya uchukuzi wa umma zitaongezeka kuanzia leo hii.
Akizungumza wakati wa mahojiano na kituo kimoja nchini, Karakacha amesema wasafiri kote nchini wanapaswa kugharamia usafiri baada ya wahudumu wa matatu kutangaza mipango ya kuongeza nauli kufuatia ongezeko la hivi punde la bei ya mafuta.
Karakacha amesema kuwa uamuzi huo unakuja kutokana na bei ya mafuta iliyotangazwa kuamkia wa kuamkia leo ambayo imesababisha gharama ya dizeli kupanda kwa Ksh40. Aidha amebainisha kuwa chama hicho leo hii, kitakuwa na mashauriano na wanachama wa chama kutoka kote nchini ili kujadili bei hizo mpya.
Chama kinashikilia kuwa ongezeko hilo ni muhimu kwa waendeshaji, lakini walikubali mzigo mkubwa wa kifedha ambao hii itaweka kwa umma. Rais alibainisha kuwa mwananchi wa kawaida ndio ataathirika zaidi, kwani watumiaji hatimaye watabeba mzigo wa kuongezeka kwa gharama za usafiri.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































