#Local News

DUALE AJIBU GACHAGUA KUHUSU SHA

Waziri wa Afya, Aden Duale, amesema hatakatishwa katika juhudi zake za kutekeleza majukumu yake, huku mvutano ukizidi kati yake na aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, kuhusu usimamizi wa mamlaka ya afya ya jamii (SHA).

Akizungumza mjini Garissa, Duale amekanusha madai ya Gachagua kwamba anahusika na ufisadi katika mfumo wa bima ya afya chini ya mpango wa huduma ya afya kwa wote, akiyataja kuwa hayana msingi.

Gachagua amekuwa akikosoa vikali SHA akidai kuwa inatumika kufuja fedha za umma, lakini Duale katika majibu yake amemsuta kwa kusambaza taarifa zisizo sahihi na kusisitiza kuwa hataruhusu kuvurugwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *