KENYA PIPELINE YALENGA UBINGWA AFRIKA
Kocha wa timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya Kenya Pipeline, Geoffrey Omondi, amesema mashindano ya vilabu barani Afrika yatakayofanyika Misri ni kiwango cha chini wanacholenga kama mabingwa wa taifa.
Omondi amesema timu hiyo ina kiu ya kutwaa ubingwa wa saba wa bara, sambamba na wawakilishi wengine wa Kenya wanaotarajia kufanya vyema katika mashindano hayo.
Kenya Pipeline itaiwakilisha nchi pamoja na wapinzani wao wa ndani, KCB na DCI, katika mashindano yatakayoanza Aprili kumi na moja hadi Aprili ishirini na nne.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































