KCB YAWEKA KIKOSI IMARA MASHINDANO YA KLABU AFRIKA
Timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya KCB chini ya kocha Japheth Munala imetangaza kikosi cha wachezaji kumi na wanne kitakachoshiriki Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika jijini Cairo, Misri.
Kikosi hicho kimejaa wachezaji wenye uzoefu mkubwa, wakiongozwa na nahodha wa muda mrefu wa timu ya taifa Mercy Moim, pamoja na Esther Mutinda, Juliana Namutira, Pauline Chemtai na Mildred Cherop.
Urejeo wa Mutinda na Cherop, ambaye amerejea baada ya kucheza kwa mwaka mmoja katika Falme za Kiarabu, unatajwa kuipa timu nguvu mpya, huku KCB ikilenga kutwaa ubingwa huo wa bara kwa mara ya tatu baada ya ushindi wao wa mwisho mwaka 2022.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































