SERIKALI YAPUNGUZA BEI YA MAFUTA
Wakenya wamepata afueni ndogo baada ya mamlaka ya kudhibiti kawi na petroli, EPRA, kupunguza bei ya mafuta ya petroli kwa shilingi 9.37 na diseli kwa shilingi 10.21, baada ya kupunguza ushuru wa thamani ya ziada, VAT kutoka asilimia 13 hadi asilimia 8.
Kulingana na EPRA, lita moja ya petroli jijini Nairobi itauzwa kwa shilingi 197.60 na diseli 196.63 huku bei ya mafuta taa ikisalia bila mabadiliko na itaendelea kuuzwa kwa shilingi 149.49.
Tangazo la EPRA linajiri baada ya Rais William Ruto hapo jana kutangaza kupunguzwa kwa bei ya mafuta ili kuwalinda wakenya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































