KPC YAZUNGUMZIA UHABA WA MAFUTA
Serikali kwa mara nyingine imetoa hakikisho kwamba kuna akiba za kutosha za mafuta nchini licha ya uhaba kuripotiwa katika baadhi ya maeneo na hata vituo kadhaa kufungwa kutokana na ukosefu wa mafuta.
Kupitia taarifa, kampuni ya Kenya Pipeline, KPC, imesema akiba zake zote zina mafuta ya kutosha kama vile diseli, petroli na mafuta ya ndege kuanzia kwenye bandari ya Mombasa, Nairobi na kwenye hifadhi za Nakuru, Eldoret na Kisumu.
Hakikisho lake linajiri huku wakenya wakitaka serikali kuweka wazi hali hali ya kiwango cha mafuta yaliyoko nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































