WANDAYI, ONE PETROLEUM WAVUTANA KUHUSU MAFUTA
Vuta nikuvute imeibuka baina ya wizara ya kawi na kampuni ya One Petroleum iliyoagiza tani 60,000 za pteroli, baada ya waziri wa kawi Opiyo Wandayi kuagiza kwamba shehena hiyo irejeshwe ilikotoka.
Hata hivyo, kampuni hiyo imepinga amri ya Wandayi, ikisema ilishinda kihalali tenda ya uagizaji mafuta, ikiwa ni miongoni mwa kampuni 4 zilizopewa tenda hiyo nje ya mfumo wa uagizaji wa kati ya serikali na serikali, G2G.
Kulingana na Wandayi, takribani shilingi bilioni 4 zingeokolewa iwapo ununuzi huo ungefanywa kupitia mfumo wa G2G.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































