#uncategorized

SHUMAH ANG’ARA, AIPA MATUMAINI TAIFA

Mshambuliaji Moses Shumah ameonyesha uwezo wake baada ya kufunga mabao mawili kwa klabu ya Power Dynamos, akiimarisha nafasi yake katika kinyang’anyiro cha mfungaji bora.

Kocha wa timu ya taifa Benni McCarthy amewahi kulalamikia ukosefu wa umakini wa kufunga mabao, hasa baada ya kupoteza nafasi nyingi katika michezo ya hivi karibuni, hali inayozua swali iwapo Shumah anaweza kuwa suluhisho.

Shumah ameendelea kung’ara aliposaidia timu yake kushinda mabao matatu kwa bila dhidi ya Mines United, akionyesha kuwa anaweza kuwa tegemeo muhimu kwa kikosi cha taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *