#Basketball #Sports

LUKENYA, KAMUSINGA ZAWIKA KWENYE VIKAPU

Shule za Lukenya na Friends School Kamusinga zilitawala mchezo wa vikapu katika mashindano ya kitaifa ya shule za upili kwa muhula wa kwanza yanayoendelea katika kaunti ya Kisumu.

Shule hizo zilifuzu semi fainali za mashindano hayo kwa mchezo wa vikapu wa wachezaji 5 kila upande yaani 5×5, Lukenya wakiilaza Dagoretti 79-62 huku Kamusinga wakiibebesha Sabunley vikapu 82-34.

Wenyeji St. Mary’s Yala pia walidumisha rekodi yao ya kutokupoteza mechi, wakiilaza Mang’u 74-49 kutinga semi fainali.

Kwa upande wa wasichana, mabingwa watetezi Butere Girls, Kaya Tiwi na St. Brigid’s walifuzu semi fainali kufuatia ushindi wao.

Butere waliitandika Takaba 105-14, Kaya Tiwi wakaicharaza Barchondo 74-51 nao St. Brigid’s wakiibandua Olympic 59-58 katika mtanange wa kufa kupona.

Katika raga ya wachezaji 15 kila upande, mabingwa wa kihistoria Kakamega High walifufua matumaini ya nusu fainali kufuatia ushindi wa 33-14 dhidi ya Menengai katika uwanja wa Jomo Kenyatta mtaani Mamboleo.

Mabingwa wa Afrika Mashariki, Kisii School, wangali wanaongoza Pool B baada ya kuicharaza Mang’u 17-6, wakiwa na pointi 8 huku Kakamega wakifuata kwa pointi 6.

Menengai ni ya 3 kwa pointi 5 huku Mang’u wakisalia bila pointi.

Katika Pool A, mibabe wa Nairobi Upper Hill walitinga nusu fainali baada ya kuibandua St. Mary’s yala 17-10, na watachuana na All Saints waliowacharaza Kwale Boys 13-12.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

LUKENYA, KAMUSINGA ZAWIKA KWENYE VIKAPU

WATTANGA ATEULIWA BAADA YA KRA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *