IEBC YAONGEZA MATAYARISHO YA UCHAGUZI
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imeimarisha matayarisho ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 kupitia kongamano la washikadau kuhusu usajili unaoendelea wa wapigakura lililofanyika Kiambu.
Kongamano hilo limewaleta pamoja wadau mbalimbali kujadili mbinu bora za kuongeza idadi ya wapigakura wanaojiandikisha na kuboresha mchakato wa usajili nchini.
Tume hiyo imesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wote ili kuhakikisha uchaguzi wa 2027 unafanyika kwa uwazi, ufanisi na ushiriki mpana wa wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































