WATU 20 WAANDIKISHA TAARIFA NA DCI KUHUSU SAKATA YA MAFUTA
Uchunguzi katika Sakata ya mafuya yenye thamani ya shilingi bilioni 2.9 umeshika kasi, jumla ya watu 20 wakiwa wameandikisha taarifa na idara ya upelelezi wa jinai, DCI.
Haya yanajiri huku washukiwa watatu ambao ni Mohammed Liban, Joe Sang na Daniel Kiptoo wakitarajiwa mahakamani leo baada ya kupewa bondi ya polisi hapo jana.
Mawakili wao wametoa stakabadhi kuonyesha kuwa maagizo ya uagizaji wa mafuta hayo yalitoka kwa kamati kuu ya baraza la usalama nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































