MSICHANA WA MIAKA 13 APATIKANA AMEFARIKI MAU SUMMIT
Wakazi wa Kijiji cha Casino eneo la Mau Summit wanaomboleza baada ya mwili wa msichana wa miaka 13 kupatikana ndani ya bwawa, tukio linaloshukiwa kuwa mauaji.
Msichana huyo aliyetambulika kama Lilian Njambi alionekana mara ya mwisho Jumatatu akicheza na wenzake kabla ya kutoweka jioni, hali iliyosababisha familia na wakazi kuanza msako wa kumtafuta.
Mwili wake umepatikana ukiwa na dalili za kunyongwa, jambo lililozua hofu kuwa huenda aliuawa kabla ya kutupwa majini, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukweli wa tukio hilo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































