#Local News

WALIMU WAKOSOA MFUMO WA SHA

Viongozi wa vyama vya walimu KNUT, KUPPET NA JSS katika Kaunti ya Nandi wamekosoa vikali mfumo wa Bima ya afya ya Jamii (SHA) wakisema una changamoto nyingi.

Viongozi hao Wamesema mfumo huo unakumbwa na matatizo kama ucheleweshaji wa huduma, ukosefu wa uwazi na changamoto katika upatikanaji wa matibabu bora, hali inayowaathiri walimu pamoja na familia zao.

Aidha, viongozi hao wametoa wito kwa serikali kurejesha bima ya AON Minet wakidai ilikuwa na ufanisi zaidi, huku wakisisitiza mageuzi ya kina ili kuboresha huduma za afya kwa walimu na watumishi wa umma.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *