#Football #Sports

HOMEBOYZ NA ULINZI STARS KUINGIA KWENYE VITA YA KOMBE

Kakamega Homeboyz watachuana na Ulinzi Stars Jumapili katika hatua ya kumi na sita bora ya Kombe la Mozzart Bet kwenye uwanja wa Bukhungu, katika mechi yenye ushindani mkali.

Mechi hiyo inazikutanisha timu mbili zenye hali tofauti za ligi lakini zenye azma sawa katika mashindano ya kombe, ambapo ushindi utawapa nafasi ya kusonga hatua ya robo fainali na kusogea karibu na ndoto za mashindano ya kimataifa.

Kakamega Homeboyz wanaingia katika mechi hiyo wakiwa katika hali nzuri ya ligi, wakishika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Kenya wakiwa na alama arobaini na sita, na wakitoka sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Nairobi United.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

HOMEBOYZ NA ULINZI STARS KUINGIA KWENYE VITA YA KOMBE

DE ZERBI MBIONI KUIKWAMUA SPURS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *