WASHUKIWA WA MAFUTA WATARAJIWA MAHAKAMANI
Washukiwa wakuu 3 wa Sakata ya mafuta yenye thamani ya shilingi bilioni 2.9 ambao ni Mohammed Liban, Daniel Kiptoo na Joe Sang wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo baada ya kukamatwa mwishoni mwa wiki jana na kuachiwa kwa dhamana ya polisi hapo jana.
Kulingana na stakabadhi zilizowasilishwa na mawakili wao, watatu hao waliagiza mafuta hayo kwa maagizo ya kamati kuu ya baraza la usalama la kitaifa na wala si kwa maamuzi yao wenyewe.
Haya yanajiri huku viongozi wa Kenya Kwanza wakionya dhidi ya siasa kuingizwa kwenye uchunguzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































