AFCON 2027: KENYA, UGANDA NA TANZANIA KUZINDUA MWONGOZO
Mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania yatazindua mwongozo utakaofuatwa katika kuandaa dimba la mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao, AFCON 2027 litakaloandaliwa katika mataifa hayo.
Waziri wa michezo Salim Mvurya, amesema mkutano kuhusu uzinduzi huo uliopewa jina la Pamoja Summit, utawaleta pamoja mawaziri Alhamisi wiki ijayo kujadili kuhusu masuala muhimu ikiwemo utoaji wa visa za usafiri na kuondolewa kwa ushuru miongoni mwa mataifa hayo kabla ya dimba hilo kuandaliwa.
Alikuwa akizungumza jijini Nairobi kwenye mkutano na kaimu katibu mkuu wa shirikisho la CAF Samson Adamu, Mvurya akikariri kujitolea kwa serikali kuandaa mashindano hayo kwa kiwango cha aina yake.
Wakati uo huo, aliongoza hafla ya kuwakaribisha afisini viongozi wapya wa kamati andalizi ya AFCON hapa nchini, akiwemo Mwenyekiti Nicholas Musonye na afisa mkuu mtendaji Antony Lungaho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































