#Local News

WANDAYI AHOJIWA KUHUSU MAFUTA DUNI

Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi amehojiwa na kamati ya bunge kuhusu madai ya uagizaji wa mafuta ya viwango duni nchini.

Kamati hiyo imeanza uchunguzi wa kina kubaini namna mafuta hayo yaliingizwa nchini na hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika katika kashfa hiyo.

Wandayi amesema mafuta hayo yalirudishwa na kusisitiza kuwa ndiye aliyemuarifu Rais William Samoei Ruto kuhusu kuwepo kwa mafuta yasiyokidhi viwango.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *