#Local News

WIZARA YA KAWI ILIJUA MAFUTA GHUSHI, SENETI YAAMBIWA

Imeibuka kwamba serikali ilikuwa na ufahamu kuhusu uagizaji wa mafuta tata tangu hatua za mwanzo, kabla ya mafuta hayo kuamrishwa kuondolewa nchini kwa kukosa kukidhi viwango na kulisababishia taifa hasara ya mabilioni ya pesa.

Akiwa mbele ya seneti, meneja mkuu wa kampuni ya Oryx Kenya Limited Angeline Maangi, amesema kampuni hiyo ilipata ombi la haraka kusambaza mafuta ya PMS ili kusaidia sekta ya mafuta nchini, na kwamba waliwasilisha kandarasi ndani ya saa 2 na kukubaliwa katika muda wa siku 7.

Maseneta wameibua maswali kuhusu hatua ya serikali kusitisha mktaba huo baadaye.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *