#Local News

HOFU YAWAKUMBA WAFANYABIASHARA KUHUSU WIZI WA KUTISHA

Wafanyabiashara katikati mwa jiji la Nairobi wameingiwa na hofu ya kiusalama baada ya genge la majambazi kuvunja duka moja la vifaa vya kielektroniki na kutoweka na bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.

Kamera za CCTV eneo hilo ziliwanasa washukiwa wakizungumza na walinzi ila baadaye walinzi wanaonekana kupoteza fahamu kabla ya wizi huo kutekelezwa, mmiliki wa duka hilo Moses Mwangi akisema nyingi ya bidhaa zilikuwa za mkopo.

Polisi kutoka kituo cha Central wameanzisha uchunguzi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *