KILIMO CHA PARACHICHI NCHINI KUFAIDIKA NA SERA YA USHURU SIFURI YA CHINA
Mnyororo wa thamani wa parachichi nchini Kenya, unaoanzia kwa wakulima, wavunaji, wachakataji na wauzaji, una matarajio mazuri kwamba, sera ya ushuru sifuri itakayoanza kutekelezwa Mei Mosi, 2026, itafungua fursa muhimu kwa sekta hiyo.
Kenya, nchi inayoongoza kwa mauzo ya nje ya parachichi aina ya Hass, ni kati ya nchi 53 za Afrika zinazotarajiwa kufaidika na sera hiyo itakayowawezesha kuingia kwenye soko la China, hatua inayoboresha ushindani na thamani ya mauzo yake.
Afisa mwandamizi mkuu wa Jamii ya Wakulima wa Parachichi nchini Kenya Ernest Muthomi amepongeza hatua ya kuondoa ushuru, akisema itachochea mauzo ya zao hilo nchini China na kuleta faida kwa wakulima na wavunaji wa Kenya.
Aidha ameongeza kuwa, kampuni kadhaa za China tayari zimeanzisha viwanda vya uchakataji nchini Kenya kuzalisha mafuta ya parachichi kwa ajili ya kuuza nchini China, na kutoa nafasi za ajira na kuongeza thamani katika sekta hiyo.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































