SENEGAL YAPIGA MARUFUKU SAFARI ZISIZO ZA LAZIMA
Serikali ya Senegal imewapiga marufuku mawaziri wake kufanya safari za nje zisizo za lazima kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na mgogoro wa Mashariki ya kati.
Akizungumza katika mkutano wa vijana Waziri Mkuu Ousmane Sonko amesema kuwa gharama ya pipa la mafuta imekaribia mara mbili ya kiwango kilichokuwa kimepangwa kwenye bajeti.
Sonko ameahirisha safari zake kwenda Niger, Hispania na Ufaransa kama sehemu ya hatua hizo, akibainisha kuwa Waziri wa Madini atatangaza hatua zaidi za kupunguza matumizi ya serikali katika wiki ijayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































