DCI, EACC ZATAKIWA KUWACHUNGUZA MAGAVANA KAIDI
Kamati ya seneti kuhusu uhasibu wa fedha za umma imependekeza idara ya upelelezi wa jinai, DCI, na tume ya maadili na kukabili ufisadi, EACC kuchunguza uwezekano wa ufujaji wa fedha katika kaunti ambazo magavana wake walishindwa kujibu maswali kuhusu uhasibu wa fedha.
Chini ya mwenyekiti wake Moses Kajwang’, kamati hiyo imewasilisha ripoti yake, ikipendekeza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya magavana hao, akiwemo Jeremiah Lomurkai wa Turkana aliyeshindwa kueleza matumizi ya shilingi milioni 22 zilizotumika kuwalipa mawakili.
Mwingine ni gavana wa Tana River Godana Dadho, anayetuhumiwa kwa madai ya kuwalipa mawakili bila uwepo wa kesi yoyote mahakamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































