#Local News

DCI YACHUNGUZA UVAMIZI DHIDI YA OSOTSI

Idara ya upelelezi wa jinai DCI imeanzisha uchunguzi katika tukio la kutamausha ambapo seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi alishambuliwa na watu wasiojulikana katika jumba moja la kibiashara jijini Kisumu hapo jana.

Kupitia taarifa, DCI imeshutumu tukio hilo, na kuongeza kuwa maafisa wake wameanzisha uchunguzi rasmi, na kwamba hadi sasa kiini cha uvamizi huo bado hakijabainika, ingawa ripoti za awali zimearifu kuwa wavamizi walikuwa wakimshutumu kutokana na msimamo wake wa kisiasa.

Kwa sasa anatibiwa katika hospitali moja jijini Nairobi huku wandani wake wakishutumu uvamizi dhidi yake.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DCI YACHUNGUZA UVAMIZI DHIDI YA OSOTSI

WATTANGA ATEULIWA BAADA YA KRA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *