RUTO AZINDUA UJENZI WA SOKO LA IKONGE, NYAMIRA
Shughuli za kibiashara katika eneo bunge la Mugirango North kaunti ya Nyamira zinatarajiwa kuimarika katika siku zijazo kufuatia uzinduzi wa ujenzi wa soko la Ikonge huku Rais William Ruto akisema shilingi bilioni 15 zimetengewa ujenzi wa masoko ya kisasa na nyumba za bei nafuu kwenye kaunti hiyo.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, Rais Ruto ambaye ameandamana na naibu wake Kithire Kindiki, ameahidi ujenzi wa miradi mingine kama vile barabara, uwanja wa michezo na reli.
Rais yuko kwenye ziara ya siku 4 katika eneo la Gusii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































