#Local News

WASHTAKIWA KWENYE KESI YA MUCHAI WAHUKUMIWA KIFO

Washtakiwa wanne waliohusishwa na mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kabete George Muchai mnamo mwaka wa 2015, wamepewa hudukumu ya kifo huku wenzao wawili wakihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kila mmoja.

Hakimu mkuu Lucas Onyina, alitoa uamuzi huo hapo jana baada ya kuwapata 6 hao na hatia ya mashataka kadhaa ikiwemo wizi wa kimabavu na kumiliki silaha kinyume na sheria.

Hata hivyo, wakili wa mshtakiwa wa pili Danstan Omari, amesema atakata rufaa katika mahakama ya upeo dhidi ya uamuzi huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *