WAUGUZI, WAKUNGA KNH WASITISHA MGOMO
Utoaji wa huduma za matibabu katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta umerejelea hali ya kawaida baada ya wauguzi kusitisha mgomo wao kufuatia mazungumzo kati ya usimamizi wa hospitali hiyo na muungano wa wauguzi na wakunga.
Akitoa tangazo hilo, Waziri wa afya Aden Duale amesema mkataba huo uliafikiwa baada ya pande husika kujitolea kwa mazungumzo ya kutamatisha mgomo huo.
Mgomo huo ulianza Jumatatu wiki hii, wauguzi wakilalamikia masuala kadhaa ikiwemo mzigo wa kazi kutokana na uhaba wa wauguzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































