METHU ASISITIZA HAJUTII ‘KUMPASHA’ RUTO
Seneta wa Nyandarua John Methu, amekariri kuwa hajutii kauli zake zilizofasiriwa kama za kumkosea heshima Rais William Ruto wiki jana katika hafla ya mazishi kaunti hiyo, akisema alikuwa akitekeleza wajibu wake kikatiba kuhakikisha Rais anatekeleza majukumu yake.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Methu amewakosoa wanaodai alimshambulia Rais kwa maneno, na kwamba hakulenga kumkosea heshima.
Amekariri kuwa anamheshimu Rais ila hamwogopi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































