#Local News

UPINZANI WAMTAKA OMOLLO KUJIUZULU KISA SHAMBULIO LA OSOTSI

Viongozi wa upinzani wanamtaka katibu katika wizara ya usalama, Daktari Raymond Omollo, kujiuzulu kufuatia kushambuliwa kwa Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi katika hoteli moja jijini Kisumu.

Viongozi hao Wanasema idara ya usalama inafahamu wahuni wanaohusika na mashambulizi dhidi ya wanaopinga serikali, na hivyo wanapaswa kuwajibika kwa hali hiyo.

Kwa upande wake, Osotsi ameeleza yaliyotokea akisisitiza umuhimu wa hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa viongozi na wananchi kwa ujumla.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *