#Local News

BARASA ASUKUMA NAFASI YA ODM KAKAMEGA

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa ameendeleza kampeni za chama cha ODM katika kaunti hiyo akieleza sababu za Kakamega kupewa nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho.

Akizungumza Bukura, kaunti ndogo ya Lurambi, wakati wa ugawaji wa bidhaa za kilimo, Barasa alisema nafasi ya naibu kiongozi wa chama hicho inapaswa kutolewa kwa kiongozi kutoka Kakamega.

Alisisitiza kuwa kaunti hiyo ina uungwaji mkono mkubwa wa ODM kuliko maeneo mengine ya magharibi, hivyo kustahili kupewa nafasi hiyo ya juu ya uongozi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *