MAFUTA KENYA, RWANDA GHALI ZAIDI YA MAJIRANI
Imebainika kuwa bei za mafuta hapa nchini na Rwanda ziko juu ikilinganishwa na mataifa mengine katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku serikali nchini ikihusisha ongezeko la hivi punde la bei na mapigano katika ukanda wa Mashariki ya kati.
Nchini Uganda, lita moja ya petroli inauzwa kwa shilingi 188.67 za Kenya huku diseli ikiuzwa kwa shilingi 186.93, nayo lita moja ya petroli nchini Tanzania ikiuzwa kwa shilingi 190 na diseli shilingi 189, huku Rwanda ikiuza petroli kwa shilingi 203.
Haya yanajiri huku upinzani ukiitaka serikali kuondoa baadhi ya ushuru unaotozwa bidhaa za petroli la sivyo uitishe maandamano.y
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































